Skip to main content

#Play4forests

Kila Sauti inahesabika

Ulijua kuwa miti ndio mitandao asili ya kijamii? Kwa njia ile ile unayoungana na marafiki na familia yako kwenye Instagram na Tik Tok, miti imekuwa ikiwasiliana kwa kila mmoja kwa maelfu ya miaka kupitia mifumo ya mizizi inayoenea kwenye sayari yetu. Misitu inasaidiana kukuwa, kugawa virutubisho na misitu iliyo thohofika, na hata kuonya juu ya hatari.

Hivi sasa hatari ni sisi, lakini tunaweza kuwa suluhisho. Kila sauti inahesabika - onyesha kuwa unajali.

Cheza sehemu yako na ulinde misitu yetu

Kwa kutia saini, ninachukua jukumu langu na natoa wito kwa viongozi wa ulimwengu kulinda misitu kama njia yetu bora ya ulinzi dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa.

Shiriki

Shiriki ombi na mtandao wako wa kijamii, marafiki wako, familia yako, jamii yako ya wachezaji na uwasaidie kucheza sehemu yao kwa misitu.

 

Wafuasi

Tusaidie kufikia wafuasi 200,000

137,152 Wafuasi
200,000 Lengo

Kwa mara ya kwanza, tunapeleka sauti za wachezaji kwa viongozi wa ulimwengu kwenye Mkutano wa Hali ya Hewa wa UN. Kama vile kila mti wa kibinafsi unashiriki katika afya ya pamoja ya msitu, sauti yako ya kibinafsi huimarisha wito wa ulimwengu wa maisha bora ya baadaye. Pamoja tunaweza kufanya tofauti kwa misitu!

See where signatures are coming from

Misitu inatusaidia, kwa hivyo hebu tuisaidie pia

Maisha ni bora na misitu

Tunahitaji misitu

Walakini tunaipoteza kwa viwango vya mwendo kasi. Kila dakika, ukataji miti unafuta takriban kiwango cha uwanja kumi za mpira wa miguu. Bila misitu, tunapoteza mshirika wetu bora katika vita dhidi ya mabadiliko ya hali ya hewa hatari.

Misitu inatuhitaji

Kusaidia ulinzi wa misitu na urejeshwaji kwa

Kuzuia uharibifu wa hali ya hewa usiobadilika

Kusaidia kulinda jaguar, nyani mkubwa, na spishi zingine nyingi zilizo hatarini

kuunda mamilioni ya kazi za kijani kibichi


Play4Forests na hali ya hewa na ushirikiano wa misitu wa Umoja wa Mataifa (UN-REDD) na Playing for the Planet Alliance, huleta pamoja majina makubwa katika uchezaji wa video kufanya kazi kwa pamoja na kushirikisha wachezaji juu ya umuhimu wa kuhifadhi na kurejesha misitu.

UN-REDD inafanya kazi katika nchi 65 kulinda misitu kupitia vitendo kama kuzuia moto wa misitu na kusaidia watu asilia.